Azam FC imepata ushindi wake wa pili baada ya kuibuka na ushindi
wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting leo kwenye Uwanja wa Chamazi.
Azam FC ambao walianza ligi kwa kuitwanga Polisi Moro kwa mabao
3-1, imeshinda mabao hayo mawili leo, yote yakitupiwa kimiani na Mrundi, Didier
Kavumbagu ambaye sasa ana mabao manne.
Kavumbagu alifunga bao moja kwa kila kipindi na kuiwezesha kupata
pointi sita zinazoipeleka Azam FC kileleni.
Mechi haikuwa lelemama kwa kuwa Ruvu Shooting chini ya Mkenya, Tom
Olaba walikuwa wakiisumbua ngome ya Azam FC kwa kipindi kirefu.
Hata hivyo, juhudi za kutaka kusawazisha katika kipindi cha kwanza
zilshindikana, wakaenda mapumziko Azam wakiongoza bao moja na kusawazisha
kipindi cha pili, halikadhalika haikuwezekana.
VIKOSI VILIKUWA HIVI:
Aishi Manula, Shomary Kapombe/Erasto Nyoni
dk46, Gadiel Michael, David Mwantika/Said Mourad dk68, Aggrey Morris, Kipre
Balou, Himid Mao/Farid Mussa dk83, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Salum
Abubakar ‘Sure Boy’ na Kipee Tchetche.
Ruvu Shooting; Abdallah Abdallah, Said Madega, Yussuf Nguya, Salvatory Ntebe, Hamisi Kasanga, Kassim Zabi, Juma Mpakala, Ally Mkanga/Baraka Mtuwo dk64, Justin Chagula, Abdulrahman Abdulrahman na Juma Nade/Ayoub Kitala dk53.

0 COMMENTS:
Post a Comment