Jezi watakazotumia Ndanda FC
ya Mtwara kwenye Ligi Kuu Bara zimevuka.
Taarifa zinasema mdhamini
kampuni ya Bin Slum Tyres kupitia matairi yake ya Vee Rubber ametengeneza jezi
maalum aina ya Adidas kwa ajili ya timu hiyo.
Taarifa zinaeleza wadhamini
hao kupitia matairi ya Vee Rubber wanaweza kuwakabidhi Ndanda jezi hizo leo au
tayari wamefanya hivyo.
Lakini SALEHJEMBE
imefanikiwa kuzinasa jezi hizo hata kabla hazijaanikwa na wadhamini hao au
uongozi wa Ndanda ambayo ndiyo imepanda daraja.
0 COMMENTS:
Post a Comment