Chelsea imeichapa Arsenal mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu England iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Stamford Bridge jijini London.
Mechi hiyo ilijaa vituko kibao ikiwa ni pamoja na kuchelewa kuanza kwa dakika 15, pia makocha Jose Mourinho na Arsene Wenger kukwidana.
Lakini ndai ya uwanja ushindani ulikuwa juu na Eden Hazard na Diego Costa walikuwa mashujaa kwa kufunga mabao hayo mawili.
Hazard alianza kwa mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa, kabla ya Costa kumaliza kazi akiwazidi ujanja mabeki na kipa wa Arsenal.
Sasa Chelsea imekwea kileleni mwa Premier League huku Costa akizidi kupaa kwa wafungaji bora akiwa na mabao tisa.
Chelsea:
Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Schurrle, Oscar, Hazard; Costa
Szczesny, Chambers, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Wilshere, Flamini, Cazorla, Ozil, Alexis, Welbeck.
MMILIKI WA CHELSEA, ROMAN ABRAMOVICH AKISHANGILIA BAO LA COSTA. |
0 COMMENTS:
Post a Comment