MALINZI... |
Na Saleh Ally
JUZI Jumatatu, nafikiri si mbali niliandika
Metodo nikieleza namna Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilivyokuwa
likipambana kukomoa watu hasa wale wenye sauti za kulikosoa kutokana na
mwenendo wake mbovu tokea jina hilo la TFF lianze kutumika.
Nikaeleza juhudi hizo zinavyoteza nguvu
wakati mataifa mengine ya jirani kama Sudan, Malawi, DR Congo, Uganda na
mengine yanavyopambana kutaka kushinda kucheza kwenye Kombe la Mataifa Afrika.
Siku makala hiyo imetoka, ndiyo kamati ya
nidhamu ya TFF, ikatangaza kumfungia mwanasheria Dk Damas Ndumbaro,
kujishughulisha na soka kwa miaka saba, kitu ambacho ni kichekesho na moja ya
comedy bora zilizowahi kufanya na shirikisho hilo.
DK NDUMBARO... |
Kosa lake ni kwa kuwa alisimama kuzitetea
klabu za Ligi Kuu Bara ambazo zilikuwa zinapinga kudhulumiwa fedha zao za
udhamini,asilimia tano kutoka Vodacom na Azam TV!
Maana yake TFF ilitaka kuona watu wote
wanakaa kimya na yenyewe inachota fedha hizo, huenda ipate nafasi ya kuendelea
kuwa na ofisi ghorofani mjini badala ya Karume, au matumizi mengine yasiyo na
tija.
Dk Ndumbaro amekuwa mhanga wa kwanza, hii
inaonyesha mapinduzi ya soka yanakuja kwa kuwa siku zote kumshinda
anayezorotesha, lazima wako watakaoumia. Tena niseme, adhabu hiyo haina
mashiko, imetolewa na waoga wa kukosolewa, kwa madai ni kamati ya nidhamu lakini
haibadilishi kuwa imetolewa na TFF ambayo imetoa mkono wa kulia, ikapeleka
kushoto, kisha hukumu.
Mapinduzi ya mapambano, kutokubali watu
kuonewa, haki itendeke na kuhakikisha TFF hii ya sasa, iliyojaa vita badala ya
maendeleo inaacha mwenendo huu mbovu au iondoke kabisa ili ukombozi wa mpira wa
Tanzania upatikane.
Dk Ndumbaro ni mwanasheria tu, nasisitiza
ni daktari wa sheria ambaye pamoja na kuwa wakili, pia ni mwalimu wa sheria
kwenye vyuo vikuu viwili nchini.
Sasa taasisi fulani, eti inamfungia asifanye
kazi (hii si taasisi ya sheria), kwa madai kuwa yeye ni mjumbe wa bodi ya ligi.
Ajabu kabisa, sijui tunakwenda wapi na sijui kwa nini watu wamelala usingizi wa
pono kuiacha TFF itawale mdundo wa mdumange wakati inaweza kucheza bolingo tu!
Kweli Ndumbaro ni mjumbe wa bodi ya ligi,
kipengele kipi kinamzuia kufanya kazi zake za sheria? Ujumbe wa bodi si ajira,
ni jambo la kujitolea, Dk Ndumbaro, mwanasheria, daktari wa sheria, mwalimu wa
sheria, halafu asifanye kazi za sheria, inawezekana vipi!
Hawa TFF hawajisikii aibu kuona suala hilo
linafikia hapo, kwa kuwa wana hofu na mtu kama Dk Ndumbaro kwamba ni hatari kwa
‘afya’ ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi, kwenye kiti chake.
Jiulize TFF itawafungia wangapi? TFF ifanya
uadui na wangapi na itapata muda wapi wa kuendeleza mpira kwa kuwa tu haitaki
kukosolewa?
Wakati wa uongozi wa Leodeger Tenga, baadhi
ya viongozi wa TFF sasa ndiyo waliongoza kampeni za kukosoa, leo mkuki kwa
nguruwe! Wamejisahau walivyokuwa, walipotoka na hawataki kukosolewa.
Kama jambo lile lilikuwa sahihi, vipi
serikali iliingia na sasa klabu zimepewa fedha zao bila ya kukatwa? Ile ilikuwa
ni dhuluma ya waziwazi, ndiyo maana imekwama na ajabu kulikuwa na ushawishi wa
chinichini kwa baadhi ya viongozi wa klabu.
Wako viongozi walioshawishiwa kukataa
kuweka saini, kutoungana na wenzao kupinga suala la wao kukatwa fedha za
udhamini. Hawajui waendako na aliyesema klabu zilimkana Dk Ndumbaro alipotosha
kwa kuwa ukweli klabu 12 zimesaini ukiachana na baadhi waliolaghaiwa ili TFF
ishinde na kuwakata! Ajabu kabisa!
Kujitetea:
Wakati suala hilo linapelekwa kamati ya
nidhamu, kwanza halikuelezwa nani anashitaki na ilikuwa kama limefanywa
kiujanjaujanja.
Dk Ndumbaro hakutakiwa kujua nani ni
mshitaki wake na anachotakiwa kwenda kujibu kwenye kamati ya nidhamu ni kipi.
Akawakumbusha hayo, baada ya hapo
wakamueleza mshitaki ni TFF, lakini bado hakukuwa na ufafanuzi wa kutosha.
Hilo lilifanyika siku moja kabla ya
kutakiwa kwenda kwenye kamati ambalo si sahihi kisheria, vipi mtu ataandaa
utetezi wake.
Hii ni sehemu ya kuonyesha tayari kamati
hiyo ilikuwa na maagizo kutoka TFF hivyo ilichotaka ni kuonekana imesikiliza.
Iwe isiwe:
Dk Ndumbaro aliwaambia ana mualiko wa moja
ya vyuo vikuu vya Marekani, safari ambayo ameiandaa kwa zaidi ya mwezi mzima.
Kwa kuwa TFF ilitaka lazima kesi hiyo
isikilizwe na kutolewa uamuzi ambao ulikuwepo, basi hilo likafanyika na uamuzi
ukatoka, yaani upande mmoja tu ukichukua uamuzi bila kusikiliza mwingine.
Hii inaonyesha hata Dk Ndumbaro ambaye ni
mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kile Huria (Out) angebaki na
kuingia kwenye kesi hiyo, iwe isiwe ilikuwa ni lazima ashindwe!
Maadili:
Suala la Dk Ndumbaro kama walivyoeleza TFF,
halikuwa ni la kamati ya maadili, huenda wao waliona kuna wepesi ambako
wanaweza ‘wakacheza’ wanavyotaka.
Sahihi lilikuwa ni suala la maadili, vema
wangeiacha kamati ya nidhamu ikasikiliza mambo mengi ya uwanjani au waamuzi.
Unapomzungumzia kiongozi wa TFF au Bodo ya
Ligi, basi kikubwa ni maadili na hasa kwa Dk Ndumbaro, waliangalia suala la
weledi, hiyo ni maadili na si nidhamu.
Waswahili wanasema, nyuki akikaribia kufa,
huruka juu sana kuliko ilivyo kawaida yake. Akishuka chini, ndiyo safari!
kwanza na wewe ulichoandika utakuwa tu umekulupuka.."WAPAMBE WA TFF, KARIBUNI MZUNGUMZE PUMBA" unaamanisha nini watu wa kusapoti wewe au... Pumba ni hizo ulizo andika wewe... kama kakiuka maadili kwanini asipate adhabu... ndugu benjamin mkapa... alisemaga waandishi wa tanzania wengi ni mambumbumbu..nafikili na wewe utakuwa mmoja wapo
ReplyDeletePumba zote tayari Ushazimaliza ww unataka zingine za nn? Wewe mwandishi usiekuwa na hata chembe ya Aibu unatoa utetezi wa upande mmoja,na wasiwasi na kalamu yako,weledi wa taaluma yako sijui kama walauu ulipita shule au ndio kipaji tena kama tulivyo wazoea,waandishi makanjanja kama ww mko wengi sana!!
ReplyDeletewewe kweli mbumbu sana, nakumbuka mtandao wako ulitumika sana kuiua club ya Simba katika uchaguzi wao na ndio leo tunaona matokeo yake, Simba uwanja hakuna tena mashimo tupu, Ushindi hakuna na mlitumika kunadi point 3 magoli matatu, mliuvunja umoja wa Simba kwa njaa zenu, na tunajua ndio nyie mnatumika kuhujumu timu ya taifa, Kasim Dewij, Hanspop, Kaburu na wengie pamoja na ndumbalo wako, kwanza inatakiwa umtete mtu kwa mazuri anayofanya, Ndumbalo alitangaza kukusanya Sahihi za ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Malinzi, Je? inahusiana na nini na madai ya vilabu? au kwa sababu mabwana zake anaowatumikia akina Dewij wamenyimwa tenda ya kuuza jezi za Taifa? Tumikeni tu kama Kondom fala nyie, harafu ndio wa kwaza kulalama mpira unakufa, mnaboa fala nyie waandishi makanjanja
ReplyDeletekumekucha
ReplyDeleteNilisema mimi huyu Saleh katumwa kwa vijisenti vya vitumbua tuu,aibu iliyoje eti mwandishi wa habari bora ungekuwa pumba wa habari!
ReplyDeleteMshika peni unakuwa huna hata ABC za uandishi,jamani huko TSJ mlienda kufanya nini?
Najua tatizo lako ni division 4 uliyoipata kidato cha nne na hukubahatika kusoma tena zaidi ya Shigongo kukupeleka nje ukajiendeleze kutengeneza udaku tuu!
Kifungo cha Ndumbaro’ ni funzo zuri kwa watu ambao wanakurupuka na kujiona wanaweza kufanya kila jambo hata kama ni kinyume cha Sheria. Ndumbaro na aendee jela ya soka sasa sababu, Tanzania bado hakuna mfano sahihi wa kuutolea endapo watu wakiwa wakivnja kanuni au sheria za mchezo wenyewe.
ReplyDeleteSoka la Tanzania linaendeshwa katika hulka za kishabiki, si wadau, mashabiki, viongozi, katika mpira wa Tanzania hakuna ‘ ukweli’ na kama upo ‘ hufichwa’.. Hivi mtu mwenye taaluma yake kama Ndumbaro anaweza kuitisha mkutano na vyombo vya habari na kutangaza kutokuwa na imani na rais wa TFF, ndugu, Jamal Malinzi?. Mwenyewe alisema ameagizwa na klabu kwa kuwa yeye ndiye muwakilishi wa klabu hizo katika mambo ya kisheria kupitia Bodi ya Ligi kuu, lakini kilichokuja kumtokea sasa ni kitu kibaya .
Klabu zimemkana lakini kuna madai zimefanya hivyo baada ya kugundua ni kosa la kinidhamu kupingana na uamuzi wa Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka. HIli kujitoa katika ‘ soo’ hilo klabu zimekataa kumuagiza, Ndumbaro kuzungumzia suala hilo. Kwa maana rahisi ni kwamba, klabu na Ndumbaro hazikukaa na kufikia uamuzi ambao ulipaswa kupelekwa kwa TFF, na badala yake, Ndu,baro alichukua uamuzi huo kama ‘ yeye’ mwenyewe alivyotafsiri sheria. Katika hili haiwezekana kusema kuwa ‘ hakutumwa’, alitumwa lakini ‘ ametengwa’ na ‘ wataalamu’ wa ‘ fitina katika soka’ na amekosa sehemu ya kushikilia.
Baada ya kupewa nafasi ya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba, Ndumbaro alishindana mambo mengi ya kisheria na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais, Ndugu, Michael Wambura. Licha ya Wambura kupewa fomu, kuijaza na kuirudisha, vigezo ambavyo vilitosha kumfanya kuwa mwanachama wa klabu hiyo, Ndumbaro aliweka ngumu suala hilo lilipofika katika nafasi yake na akatumia ‘ mwanya huo’ kumuumiza Wambura na kumuondoa katika uchaguzi kwa sababu zilizotengenezwa na mahasimu wake kuelekea katika uchaguzi huo. Wakati ule Ndumbaro, alivumba huku akimuita ‘ Wambura, ni mtoto katika mambo ya sheria’ huku akimuita mwanafunzi wake.
Alishinda wakati ule lakini ameanguka vibaya mbele ya jam,bo ambalo hakupaswa kulisema baada ya kutegwa na ‘ watu wake’. Alitaka kubatilisha maamuzi ya kamati ya utendaji ya TFF, ni kosa la kisheria licha ya yeye kuwa mwanasheria haikumsaidia kujua hilo na badala yake ‘ akalazimishwa kufanya makosa’ yaliyomchukua peke yake. Kuna kitu kinaendelea hapa, na mengi yatajitokeza sasa kuhusu ukaribu wa Ndumbaro na baadhi ya watu wa mpira nchini ambao ‘ wamemsariti’ huku akivunja Sheria za soka.
Katika hili naipa pongezi TFF kwa kuchukua uamuzi mgumu, sgeria ziendelee kutumika na kufanya kazi. Kama hakutumwa kwa nini alizungumza? Kuna methali ya Kiswahili husema; ‘ Muosha, huoshwa’.