Mechi nne za Kundi A la Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Timu za African Lyon na Kimondo FC
ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini
mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
Nayo mechi ya Polisi Dar es Salaam na
Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar
es Salaam, sasa itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mechi ya Friends Rangers na Ashanti
United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani, Oktoba 26 mwaka huu, sasa
itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka huu.
Pia mechi ya Lipuli FC na JKT Mlale
iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa,
imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu
kwenye uwanja huo huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment