Pamoja na kufungwa mechi mbili mfululizo
kati ya tatu walizocheza na kuibuka na ushindi mchezo mmoja, Ndanda FC na
Mtibwa Sugar ni timu pekee zilizoweza kufunga mabao sita katika michezo yao
yote mitatu ya ligi kuu.
Ndanda mpaka sasa inashikilia nafasi ya tisa
ikiwa na pointi tatu ambapo katika mchezo wa kwanza ilikuwa ikiongoza ligi.
Klabu hiyo ilifanikiwa kufunga mabao manne
katika mchezo mmoja dhidi ya Stand United, lakini mengine yaliweza kupatikana
katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kuchapwa mabao 3-1 na dhidi ya
Coastal 2-1 na kuweza kufikisha idadi ya mabao sita.
Ingawa kinara katika msimamo wa ligi Mtibwa
pia ana mabao sita yenyewe imeshinda michezo yake yote mitatu tofauti na Ndanda
huku klabu ambazo zinaongoza kuwa na mabao machache kuliko zote zikiwa ni
pamoja na Mbeya
City, JKT Ruvu na Mgambo JKT, zote zina bao moja-moja na Ruvu Shooting haina
bao hata moja.
Simba na Yanga zote zimefunga mabao
manne-manne na kufungwa idadi hiyohiyo ya maba
0 COMMENTS:
Post a Comment