Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni amekutwa na mkasa mkubwa
baada ya kumgonga dereva bodaboda katika eneo la Tip Top Manzese lakini akaendelea kukimbia akiyagonga baadhi ya magari hadi katika eneo la Kijitonyama jijini Dar ambako alikwama baada ya kuligonga gari la Global Publishers.
Baada ya tukio hilo, Nyoni, beki wa Taifa Stars alitoka kwenye gari lake aina ya Toyota Grande Mark 11 GX 110, akaanza kujitahidi kukimbia kutokana
na lundo la bodaboda kuanza kumfukuza wakitaka kuchukua sheria mkononi, hali iliyomtia hofu.
Walimfukuza hadi kufika eneo la Kijitonyama ambako
alikwama baada ya kuligonga gari hilo la GPL na alipoteremka kwenye gari, wakaanza kumshambulia kama mwizi.
Nyoni alishambuliwa na lundo la madereva Bodaboda,
lakini akafanikiwa kukimbia huku wakiendelea kumpiga na hata watu walipojitokeza kumsaidia, waliendelea kumpiga bila huruma.
Kwa mujibu wa walioshuhudia, Nyoni alishambuliwa kama
mwizi katika eneo la tukio huku zaidi ya watu 30 wakimpiga.
Beki huyo wa Azam FC alionekana kama anakimbilia kituo cha Polisi cha Kijitonyama Mabatini, lakini hakufanya hivyo na madereva hao wa Bodaboda walipomnasa walikuwa wakimshambulia kama mwizi naye alijaribu kujitetea na alipozidiwa, alitokomea kusikojulikana.

0 COMMENTS:
Post a Comment