TIMU ya Barcelona inatarajia kumtia kitanzi kingine mshambuliaji wao hatari kwa kutupia Lionel Messi mwenye umri wa miaka 32.
Mabosi wa timu hiyo wanataka kumuongezea mkataba ambao utambakiza Messi ndani ya Neo Camp kwa miaka iliyosalia ya soka lake.
Rais wa Barcelona Jose Maria Bartomeu amesema kuwa
Messi anatarajia kumaliza mkataba wake na utamruhusu yeye kuondoka Barcelona bure.
Barcelona wanaamini kuwa watambakiza nyota huyo hadi 2022 na baada ya hapo sasa ataruhusiwa kuondoka Neo Camp.
Inadhaniwa kuwa huenda nyota huyo atarudi kucheza nchini kwao Argentina kunako klabu yake ya zamani ya utotoni Newll's Old Boys kabla ya kustaafu kandanda.
Mazungumzo ya mkataba huo yanatarajia kuanza mapema iwezekanavyo mwezi ujao. Na mkataba huo utamruhusu kuondoka klabuni kwa muda.
0 COMMENTS:
Post a Comment