Na Saleh Ally
KOCHA Kim Poulsen amefunguka kwa mara ya
kwanza na kuweka wazi kuwa amefanya mazungumzo na Simba.
Poulsen raia wa Denmark, amefanya mahojiano
maalum na Championi Jumatano, jana mchana na kusema anaangalia kati ya ofa
mbili, moja ya Simba na pili kwao Denmark na bado hajafikia uamuzi sahihi.
Awali, gazeti hili liliandika kuhusiana na ujio
wa Poulsen aliyewahi kuinoa Taifa Stars, lakini mmoja wa viongozi wa Simba akatumia
nguvu nyingi bila sababu kukanusha vikali kwamba hawajui lolote kuhusiana na
kocha huyo.
Akizungumza kutoka katika jiji la Windhoek
ambao ni mji mkuu wa Namibia, Poulsen alisema ndani ya siku chache atakuwa na
jibu sahihi.
SALEHJEMBE: Dar es Salaam unatarajia kuwasili lini?
Kim:
Bado kidogo, sijajua maana Simba ndiyo wanaweza kulizungumzia hilo.
SALEHJEMBE: Labda mmefikia wapi katika mazungumzo yenu?
Kim:
Tumefikia pazuri, naamini nina nafasi ya kufanya kazi tena Tanzania. Lakini
hili wanaweza kulizungumzia wao. Kwangu wakati haujafika.
SALEHJEMBE: Umesema una ofa nyingne, ni wapi?
Kim:
Nyumbani Denmark. Lakini huwezi kujua labda inaweza kuja nyingine kutoka Asia
au kwingine. Ila sasa naendelea kuangalia kuhusiana na Simba na hiyo timu ya
Denmark.
SALEHJEMBE: Umesema uko Namibia, kunani?
Kim:
Ndiyo, sasa ni mkufunzi wa Fifa, nawafundisha makocha wa timu za ligi kuu.
Nilianzia Lesotho, wiki iliyopita.
SALEHJEMBE: Sawa karibu Tanzania.
Kim:
Ahsante, Championi linaendeleaje.
SALEHJEMBE:
Tunaendelea kukimbiza kama kawaida yetu.
Kim:
Hongereni, naijua kazi yenu, nashukuru kwa kunitafuta. Kila la kheri.
Poulsen ni kati ya makocha wanaosifika sana
kuhusiana na suala la kuwakuza na kuwainua vijana na Simon Msuva wa Yanga na
Frank Domayo wa Azam FC ni kati ya aliowapa nafasi kubwa ya kukua kimpira.
0 COMMENTS:
Post a Comment