Bayern
Munich ndiyo timu tajiri zaidi nchini Ujerumani na kama utazungumzia kwa
ujumla, basi Bundesliga ndiyo ligi ghali zaidi kifedha barani Ulaya.
Ukitaka
uhakikishe hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bayern maarufu kama Bavarian, Karl-Heinz
Rummenigge amesema wameishalipa fedha zote walizokuwa wakidaiwa kwenye uwanja
wao.
Uwanja
wa The Allianz Arena uliojengwa mwaka 2005, umewagharimu kitita cha euro 346 na
walitakiwa kulimaliza deni hilo mwaka 2030.
Kutokana
na fedha nyingi wanazoingiza, Bayern tayari wamelipa deni lote.
Hali hiyo
imewashangaza wataalamu wengi wa masuala ya uchumi.
Awali
uwanja huo ulikuwa ukimilikiwa kwa pamoja na Bayern na 1860 Munich, lakini sasa Bayern inaumiliki kwa 100%.
0 COMMENTS:
Post a Comment