December 20, 2014

 
KIKOSI CHA MWADUI FC

Kocha Mkuu wa Mwadui FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amekubali kuwa Simba kweli ni wazuri.


Simba imecheza mechi ya kirafiki leo dhidi ya Simba na kulala kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

"Nikubali Simba ni wazuri, wamecheza vizuri na kutupa wakati mgumu. Ni timu iliyokaa pamoja na ina wachezaji wengi vijana.

"Nimeona kuna wachezaji wageni, lakini wengi ni vijana ambao wametokea timu b.
"Hata kama tumefungwa tatu, lakini mpira ulikuwa mzuri na sisi imetusaidia maana tumecheza mechi nyingi mfululizo, ni zaidi ya mechi nne.

"Hivyo tunaweza kuwa tumefaidika na mengi na waliokuja uwanjani wamefurahi kutokana na soka safi timu zote zimeonyesha," alisema Julio.

Kabla ya mechi hiyo, Julio alitamba ataionyesha kazi Simba ili wajue amekuwa akifukuzwa kwa mizengwe tu lakini uwezo anao.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic