RAIS WA TFF, JAMAL MALINZI. |
Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema imepokea
kwa masikitiko taarifa za masuala ya mpira wa miguu Zanzibar kupelekwa
mahakamani.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za uendeshaji mpira wa miguu ambazo
zinakataza masuala ya mchezo huo kupelekwa katika mahakama za kawaida.
Katika taarifa iliyotolewa leo na TFF, imeeleza kuwa jambo hilo si
sahihi.
Kamati ya Utendaji inatoa rai kwa pande zote mbili zinazohusika na
mgogoro huo kukaa kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza tofauti zao.
Kamati ya Utendaji imejitolea kutuma ujumbe wake Zanzibar ili
ukutane na pande zinazohusika katika mgogoro huo.
Ni muhimu usuluhisho upatikane haraka ili tuweze kujua hatma ya
washiriki wetu kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment