Yule beki aliyemkaba koo mshambuliaji wa
Yanga, Amissi Tambwe hivi karibuni, George Ossei Michael, ameibuka tena na
kuzua gumzo baada ya kumgonga mshambuliaji wa Stand United, Pastori Anathans na
kumfanya apoteze fahamu.
Tukio hilo lilitokea katika mchezo wa Ruvu
dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani Jumapili iliyopita na
kuchezeshwa na mwamuzi Kennedy Mapunda.
Katika mchezo huo, Ruvu iliibuka na ushindi wa
mabao 2-1.
Mkurugenzi wa Ufundi wa
Stand, Muhibu Kanu, amesema kuwa wamesikitishwa na kitendo cha mchezaji wao
kujeruhiwa na refa kutochukua uamuzi wowote.
“Sipendi
kuongelea waamuzi, lakini yule wa juzi alinishangaza kidogo, mchezaji anagongwa
mpaka kupoteza fahamu yeye hachukui hatua yoyote, wengi wamezabwa vibao
hakuchukua hatua yoyote.
“Beki wao yule George alikuwa anacheza rafu
sana na ndiye aliyesababisha Pastori apoteze fahamu, mambo mengi yalitokea
katika mchezo ule, lakini yalifumbiwa macho, TFF wanatakiwa kuwa makini
kuhakikisha mambo yanakwenda sawa, wasitumie ripoti pekee, watumie hata video,”
alisema Kanu.
Kwa upande wa Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau
Bwire, alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, alifunguka kuwa yeye hakuliona.
0 COMMENTS:
Post a Comment