Uongozi wa Stand United
umeamua kupora simu za wachezaji wake kuelekea mechi ya Simba.
Stand imefikia uamuzi huo ili
kuhakikisha hakuna hujuma kabla ya kuwavaa Simba kesho kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga.
Habari za ndani kutoka Stand
United zinaeleza kila mchezaji amekabidhi simu yake kwa uongozi.
“Wachezaji wametakiwa
kukabidhi simu kwa uongozi na hilo limefanyika kwa ajili ya uhakika tu.
“Si kwamba Simba wametuhujumu,
lakini kwa kuwa ni timu kubwa lazima tuwe makini sana katika hili,” kilieleza
chanzo.
Stand itakuwa na kazi ya
kuizuia Simba kesho ili angalau kukusanya pointi zitakazoikwamua eneo la
mkiani.
Tayari Simba iko mjini Shinyanga tayari kwa mechi hiyo inayotarajiwa kuingiza idadi kubwa ya watu.








0 COMMENTS:
Post a Comment