December 29, 2018




KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameamua kumtumia salamu kocha Mkuu, Patrick Ausems baada ya kuonyesha ufundi wa kucheka na nyavu leo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliochezwa uwanja wa Taifa kutokana na kuanzia benchi mara nyingi.

Kichuya aliwanyanyua mashabiki kwa kutoa pasi ya bao la kwanza dakika ya 17 lililofungwa na John Bocco ambaye kwa sasa anafikisha bao la tatu kwenye Ligi.

Dakika ya 49 Kichuya alifunga bao la pili akiwa ndani ya 18 kwa mguu wa kulia lililomshinda mlinda mlango wa Singida United kabla ya kulazimisha kuingia ndani ya 18 na kufunga bao la tatu dakika ya 54 kwa mguu wake wa kulia akimalizia pasi za Clytous Chama.

Licha ya kufungwa mabao hayo bado Singida United walijitahidi kufanya mashambulizi kwa kushtukiza lango la Simba hali iloyomfanya mlinda mlango Aishi Manula kuwa katika kazi nzito kuokoa jahazi la Simba na kufanikiwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic