MUSLEY AKIWA NA IVO MAPUNDA BAADA YA KWISHA KWA MECHI YA WATANI NA SIMBA KUSHINDA KWA BAO 1-0, SIKU AMBAYO TAFRANI LILIANZIA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR. |
Musley Al Rawah, mjumbe
wa kamati ya utendaji wa kamati ya Simba, amehojiwa na kuachiwa.
Kiongozi huyo amehojiwa
kuhusiana na tuhuma za kumsukuma mtoto wa mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji
wakati wakiwa kwenye lifti kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Manji alifungua mashitaka
akidai Musley alimsuma mwanaye na kumuumiza.
Wajumbe wa kamati ya
Utendaji ya Simba walikuwepo kituo cha kati jijini Dar es Salaam kufuatilia
sakata hilo la Musley.
Walijitokeza kwa wingi
kuhakikisha mwenzao huyo anatoa maelezo na baadaye ilielezwa aliwekewa dhamana
na mmoja Friends of Simba wakongwe, Crescentius Magori.
Musley hakupatikana
kulizungumzia sakata hilo, lakini taarifa zimeeleza kuwa amekuwa akisisitiza,
suala hilo lilikuwa bahati mbaya na asingeweza kumsukuma mtoto mdogo.
0 COMMENTS:
Post a Comment