Timu za Kiluvya United ya
Pwani, Mbao FC ya jijini Mwanza, Mji Njombe kutoka mkoa mpya wa Njombe na Mji
Mkuu (CDA) ya Dodoma zimepanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kuongoza
katika misimamo ya makundi yao ya Ligi Daraja la Pili (SDL).
Kwa kuzingatia Kanuni ya
5 (8) ya Ligi Daraja 9SDL Toleo la 2014, hatua ya pili Ligi Daraja la Pili
kutafuta Bingwa na sasa timu hizo zitacheza kusaka Bingwa wa ligi Daraja la
Pili.
Mji Njombe itacheza na
timu ya Kiluvya United tarehe 14 Machi mwaka huu katika uwanja wa Amani
Makambako, na mchezo wa marudiano kufanyika tarehe 18 Machi, 2015 katika uwanja
wa Mabatini Mlandizi.
Nayo Mbao FC ya Mwanza
watawakaribisha timu ya Mji Mkuu FC mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza, na mechi ya marudiano itachezwa Machi 18, 2015 katika
uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Fainali inatarajiwa
kufanyika Machi 22 mwaka huu jijin Dar es salaam (uwanja wa mchezo utatangazwa
baadae) kwa kuzikutanisha timu zilizopata pointi nyingi katika michezo hiyo
miwili ya awali.
0 COMMENTS:
Post a Comment