Bao la dakika 54 la mshambuliaji wa kimataifa
raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, limemfanya kiungo mshambuliaji wa Yanga,
Mbrazili, Andrey Coutinho aishiwe nguvu jukwaani.
Timu hizo zilivaana wiki iliyopita kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara
iliyomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa na Mganda huyo.
COUTINHO... |
Mganda huyo,alifunga bao hilo kwa shuti kali
la mita 20, lililomshinda kipa, Ally Mustapha ‘Barthez’ na kujaa wavuni.
Coutinho
alisema kuwa mara baada ya bao hilo kuingia wavuni, ghafla alishangaa kuishiwa
nguvu mwili na kujikuta akishindwa kufanya chochote.
Coutinho alisema, kipigo hicho kimemkosesha
furaha moyoni mwake kutokana na kukutana mara tatu na timu hiyo yeye akiwa hapa
nchini na kushindwa kuifunga, mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu walitoka
suluhu, Mtani Jembe walifungwa 2-0 kabla ya juzi kufungwa bao 1-0.
“Baada ya kuwakosa kwenye mechi ya mzunguko wa
kwanza ligi kuu na Mtani Jembe, nilitarajia kuona timu yangu inapata ushindi
kwenye mechi ya leo (Jumapili), lakini tukashindwa kuwafunga tena.
“Nguvu
zimeniisha ni bora tukafungwa nikiwa uwanjani nacheza, najua nisingeumia kwa
sababu nipo uwanjani nimeshindwa kuipigania timu yangu ikipata ushindi.
“Baada ya bao kuingia nilihisi kuishiwa nguvu,
nilikuwa najisikia vibaya sana, hakika sikutarajia matokeo yale,” alisema
Coutinho.
0 COMMENTS:
Post a Comment