CANNAVARO BAADA YA KUSHONWA NYUZI SABA, AKIWA NA BAADHI YA WAUGUZI WALIOMHUDUMIA... |
Beki ngangari wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
amejiondoa kwenye kikosi hicho kitakachoivaa Platinum ya Zimbabwe.
Timu hiyo, inatarajiwa kuvaana na Platinum
katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Cannavaro alisema amejiondoa kwenye kikosi
hicho baada ya kupasuka juu ya jicho la kushoto na kusababisha ashonwe nyuzi
saba.
KUMRADHI KWA PICHA: CANNAVARO WAKATI AKISHONWA... |
Cannavaro alisema, nyuzi hizo alishonwa juzi
Jumatatu asubuhi kwenye Hospitali ya Kilwa Road, Kurasini jijini Dar mara baada
ya mechi hiyo kumalizika.
Aliongeza kuwa, hataweza kucheza kutokana na
maumivu makali anayoyasikia kwenye jeraha hilo, hivyo ameona ni vyema akapumzika
hadi jeraha hilo litakapopona kabisa kwa hofu ya kujitonyesha.
“Ujue nilitumia ujasiri sana kusimama na
kuendelea kucheza mechi na Simba mara baada ya kugongana na mchezaji wa Simba
ambaye sijamjua ni nani na nilidhani nimepasuka padogo kumbe ni pakubwa.
“Niligundua nimepasuka pakubwa mara baada ya
kwenda hospitali na kugundulika jeraha ni kubwa na kutakiwa kushonwa nyuzi saba
juu ya jicho langu, nilinyanyuka kuendelea kucheza kutokana na mapenzi yangu na
Yanga.
“Nilitamani kucheza mechi na Platnum, lakini
kutokana na jeraha hili kiukweli sitaweza kucheza, nimeona nipumzike kwa kuhofia
kujitonyesha, nyuzi saba ni nyingi sana, yaani nina maumivu mara mbili ya
kukosa fedha za ahadi kama tukiifunga Simba na maumivu haya niliyoyapata,” alisema
Cannavaro kwa masikitiko makubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment