April 5, 2015

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema ana imani kubwa kikosi chake kitafanya vizuri dhidi ya Simba, leo.


Simba inakuwa mgeni wa Kagera Sugar katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Kopunovic amesema mvua ndiyo hofu yake kubwa kama zitaharibu uwanja.

“Kucheza katika mazingira ya mvua, kuna ugumu wake. Kama haitakuwa hivyo nina imani tutacheza vizuri tu.

“Kidogo nimekuwa nikiomba, mvua isinyeshe tena (kichekesho). Uwanja ukiwa umetulia ni lahisi kiuchezaji,” alisema Kopunovic raia wa Serbia.


Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu huku Simba wakitaka kulipa kisasi baada ya Simba kufungwa bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic