Mashabiki wa Yanga
waliosafiri kwenda nchini Zimbabwe kuiunga mkono timu yao ikipambana na FC
Platnum ya Zimbabwe wameonyesha ni wazalendo hasa.
Mashabiki na wanachama
hao, wameshika gurudumu la kazi ya upishi baada ya kuhakikisha wanapiga chakula
safi kwa ajili ya wachezaji wao wanaopambana leo dhidi ya FC Platnum.
Si kwamba Yanga haina
fedha, lakini hofu ya hujuma ambazo zilianza kujionyesha mapema na inaokana
Platnum inashirikiana na serikali ya Zimbabwe.
Wanachama na mashabiki
hao walifanya kazi za upishi kwa ustadi mkubwa kwa ajili ya wachezaji hao.
Tena wakati wanapika,
ulinzi ulikuwa mkali ile mbaya kuhakikisha kila kitu salama.
Baada ya hapo,
kilichofuatia ni wachezaji kupiga msosi mapema kujiandaa dhidi ya Platnum ambao
walilambwa bao 5-1 jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment