Huku Ligi Kuu
Bara inaelekea ukingoni, Kamati ya Usajili ya Simba, tayari imeanza kufanya
tathmini ya wachezaji inaowahitaji kuongeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema tayari wameshafanya tathmini kuwa wanahitaji kuongeza wachezaji katika nafasi
tatu ili kujiimarisha zaidi.
“Siwezi kukuambia
majina, lakini tutaongeza wachezaji katika nafasi tatu kwa ajili ya
kujiimarisha zaidi.
“Kwanza ni beki
wa kati, tunalazimika kujiimarisha zaidi kutokana na tulivyoona utendaji katika
nafasi hiyo.
“Hatujajua beki
atatokea nje au ndani ya Tanzania, tayari tumeanza kutafuta taratibu. Pili
tunahitaji kiungo ambaye atakuwa na uwezo wa kukaba na kuchezesha timu ili
kusaidiana na kina (Said) Ndemla na (Abdi) Banda pale kati.
“Nafasi ya tatu
ni mshambuliaji, ukiangalia inaonyesha wazi tunahitaji mtu mzuri wa kufunga,”
alisema Hans Poppe.
Alisisitiza
katika mechi chache zilizobaki, watakaa na Kocha Goran Kopunovic na kusikia ana
maoni au mapendekezo yapi.
Hadi sasa Simba
iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara na leo Jumamosi inakutana
na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment