Mshambuliaji
Mkenya wa Simba, Paul Kiongera amesema yuko safi baada ya kurejea uwanjani na
kuitumikia KCB ya Kenya ambayo ilimuuza kwa Simba.
Kiongera
aliumia goti na kutibiwa nchini India na baada ya hapo Simba ikampeleka kwa
mkopo KCB. Tayari uongozi wa Simba ulisema unamrejesha kikosini msimu ujao.
Nyota
huyo amekuwa nje akiuguza jeraha la goti alilotonesha akiitumikia Simba katika mchezo
wa ufunguzi wa ligi kuu msimu huu dhidi ya Coastal Union, kabla ya Simba
kusimamisha mkataba wake kwa muda hadi msimu ujao ambapo ameahidi kurejea
Msimbazi.
Akichonga
kutoka Nairobi, Kiongera alisema ameshakuwa fiti na kwamba atakuwa uwanjani
wiki ijayo kwa mara ya kwanza kuichezea KCB huku akitamba kuwa Kiongera ni yuleyule hata
angekaa nje mwaka mzima.
“Namshukuru
Mungu, nimepona kabisa na wiki ijayo nina uhakika wa kucheza mchezo wangu wa
kwanza katika kikosi changu cha KCB. Nipo hapa kwa mkopo-kulikuwepo makubaliano
na Simba kwamba nitakuwa hapa hadi msimu ujao. Tuombe uzima msimu ujao, naweza
kuja huko,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment