Aliyewahi kuwa mdhamini wa Coastal Union, Nassor Binslum, juzi
Jumatano alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kulazimika kuondoka uwanjani
kabla ya mchezo kumalizika kutokana na kipigo cha mabao 8-0 ilichopokea timu
hiyo kutoka kwa Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Binslum ambaye kwa sasa amerejea kuipa sapoti timu hiyo ambayo
imeanza kuyumba kwenye ligi, alikuwa uwanjani hapo akishuhudia mchezo huo ambao
haukuwa mzuri kwa upande wao.
Binslum ambaye alikuwa amekaa kwenye viti vya jukwaa kuu, aliondoka
uwanjani hapo ikiwa ni dakika ya 85 kabla ya mpira kumalizika wakiwa nyuma kwa
mabao 6-0, ambapo hakuweza kushuhudia mabao mawili ya Salum Telela na Tambwe
yaliyofungwa dakika za 87 na 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment