April 10, 2015


Simba imeanza mazungumzo na beki Said Morad ili kufanya juhudi za kumrejesha kundini.


Taarifa za ndani ya Simba zimeeleza kwamba uongozi wa klabu hiyo umepanga kujiimarisha zaidi na Morad anayekipiga Azam FC kwa sasa ni sehemu ya 'target'.

Morad mwenyewe amesema kuwa msimu ujao Mungu akijaalia atakuwa ndani ya jezi za rangi nyekundu na nyeupe ambazo huvaliwa na Simba.

“Mkataba wangu na Azam unamalizika Jumatano ijayo, hivyo baada ya hapo mimi siyo tena mchezaji wao kwani mpaka sasa tunavyoongea na wewe hawajaonyesha dalili zozote za kutaka nibakie katika kikosi hicho.

“Hakuna kiongozi yeyote aliyenifuata na kuniambia suala lolote linahusiana na mkataba, hivyo basi kutokana na hali hiyo, msimu ujao kuna uwezekano mkubwa mkaniona nikiwa ndani ya uzi wa Simba,” alisema Morad.

Morad aliwahi kuitumikia Simba mwaka 2006 akitokea Ashanti United na baada ya hapo alitimkia Kagera Sugar kisha Azam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic