Tanzania imepangwa katika Kundi G lenye timu
za Misri, Nigeria na Chad katika harakati za kuwania kucheza Kombe la Mataifa
Afrika mwaka 2017.
Kundi hilo tayari limebandikwa Kundi la Kifo
na Watanzania wengi wanaonekana kuingia hofu.
Mmoja wa wachezaji nyota wa zamani wa kikosi
cha Tanzania, Taifa Stars, Edibil Lunyamila amesema haoni sababu ya Tanzania
kuwa na hofu.
Lunyamila amesema anaamini Watanzania wana
kila sababu ya kuamini wanaweza na sasa ndiyo wakati mwafaka wa kuanza maandalizi.
“Sasa ukiihofia Misri, siku nyingine
utapangwa na Tunisia au Algeria. Au Ghana na Cameroon, vipi maisha yetu yawe ya
woga.
“Kinachotakiwa ni kuanza maandalizi ya
uhakika ili kujiandaa,” alisema Lunyamila.
Misri na Nigeria ni kati ya vigogo wa soka
la Afrika, hali inayoonekana kuwapa hofu wengi.
Kikosi cha Tanzania chini ya Mholanzi, Mart
Nooij kinaonekana kutoaminiwa na wengi kutokana na mwenendo wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment