Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema iwapo wachezaji wake wataendelea kuzitumia nafasi wanazozipata, ana uhakika watashinda mechi zote za Ligi Kuu Bara kwa idadi nzuri ya mabao.
Katika mechi yake ya Ligi Kuu Bara jana, Yanga imeibutua Coastal Union kwa mabao 8-0.
Yanga ingeweza hata kufunga mabao 12, lakini katika kipindi cha kwanza ilipoteza nafasi nyingi sana za kufunga.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Pluijm raia wa Uholanzi amesema Yanga ilikuwa na nafasi ya kushinda mechi nyingi kwa mabao mengi, lakini hawakuwa wakitumia nafasi.
"Utaona matokeo yetu kwa siku za hivi karibuni yanabadilika. Tunashinda kwa idadi nzuri ya mabao, jambo ambalo tungeweza kulifanya kwa kipindi kirefu sasa.
"Hatukuwa tukitumia nafasi tunazozipata, ndiyo maana ilikuwa tunashindwa kupata ushindi mzuri. Kama tutakuwa makini katika kutumia nafasi, ushindi hauwezi kuwa mgumu kwetu," alisema Pluijm.
Jamani,nampenda huyu kocha wa Yanga sana,hana majigambo,maongezi yake kawaida sana na ni kwamba anajua mpira ni dakika 90,ndani ya muda huo lolote laweza tokea.Sio akina Julio kila siku majigambo tuuuuuuuuuu.Yanga wamekukomesha JULIOOOOOOOOOOOOOOOO,KIMYAAAAAAAAAAA!Na sijui kama hajaugua, kwa kichapo kile!
ReplyDelete