Kiungo mkabaji wa Taifa Stars, Said Juma
Ally ‘Makapu’ ameanza safari ya kurejea nyumbani kutoka Afrika Kusini.
Makapu amerudishwa nyumbani kutokana na kuwa
majeruhi, hali iliyosababisha benchi la ufundi, kumruhusu kurejea.
Taarifa kutoka Afrika Kusini zimeeleza kuwa
tayari Makapu ametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wa
jijini Johannesburg ili kuanza safari hiyo.
Hata hivyo, Makapu anayekipiga Yanga
anarejea nyumba ikiwa tayari Stars imeng’olewa katika michuano ya Cosafa.
Stars imetolewa baada ya kipigo cha pili mfululizo
dhidi ya Madagascar. Wakati mechi ya kwanza ilianza kuchapwa na Swaziland.
0 COMMENTS:
Post a Comment