Kama kweli Kocha Mart Nooij ataendelea
kubaki na kuifundisha Tanzania, itakuwa sehemu ya mijiza ya soka.
Taifa Stars imepoteza mchezo wake wa pili
kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar. Kipigo cha kwanza kilikuwa ni bao
1-0 dhidi ya Swaziland.
Mechi mbili, Taifa Stars haina pointi wala
bao. Tena kama utazungumzia msimamo wa ubora wa Fifa, Stars iko juu ya timu
zote.
Inawezekana kabisa Cosafa walijua Stars ina
ubora wa juu kutokana na rekodi zake.
Walitoa mwaliko wakitemea ushindani na soka
lenye mvuto. Lakini Stars imeonyesha kabisa haichezi kitimu.
Kocha huyo Mholanzi mbishi, mwenye sura ya
kiburi na majibu ya nyodo, ndiye chanzo.
Stars imeshindwa kuonyesha soka la kuvutia. Stars
imeshindwa kuonyesha ni timu yenye kocha anayelipwa mamilioni ya Watanzania.
Uwezo aliouonyesha Nooij hauna tofauti hata
kidogo na makocha wetu wa wazawa, tena huenda wako wanaomzidi.
Nafikiri huu ndiyo wakati mwafaka wa babu
huyo wa Kiholanzi kuiacha Stars akatafute sehemu nyingine anakoweza kuwafanyia
utani na kazi.
Jamaa ana matatizo kuanzia uteuzi hadi ufundishaji. Hana mfumo wala program zozote ziwe za muda mrefu wala mfupi!! Tumemvumilia sana, hawezi tupeleka popote
ReplyDelete