Kocha Dick Advocaat alijikuta akimwaga chozi
baada ya sare ya bila kufungana dhidi
ya Arsenal, jana.
Sare hiyo imeibakiza Sunderland katika Ligi
Kuu England.
Sherehe za Sunderland zilianza palepale
uwanjani huku wachezaji na kocha wakionekana kuchanganyikiwa kwa furaha.
Hata hivyo, Sunderland walilazimika kutumia
nguvu ya ziada kubaki nyuma kwa ajili ya kujilinda ili kuhakikisha wanamaliza
mechi hiyo angalau kwa sare.
0 COMMENTS:
Post a Comment