DANGOTE... |
Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na
bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa
mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.
Dangote, raia wa Nigeria,
kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea,
anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na
hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.
Mwenyekiti wa Ndanda FC,
Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big
Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji
kwenye mkoa wao.
“Tunafikiria kufanya
mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu
ambayo imenusurika kushuka daraja.
“Unajua tangu ligi
imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali
basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi
hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike
kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.
0 COMMENTS:
Post a Comment