Siku chache baada ya Yanga kudaiwa kuwa ina
mpango wa kuwatema nyota wake 11 wa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix
Minziro, ameibuka na kuomba apatiwe wachezaji hao.
Baadhi ya wachezaji ambao Yanga inadaiwa kutaka
kuwafungashia virago klabuni hapo ni Jerry Tegete, Hussein Javu, Danny Mrwanda,
Nizar Khalfan, Rajabu Zahir, Edward Charles na Hassan Dilunga.
Sababu kubwa Yanga kufanya hivyo ni kutokana na
wachezaji hao kushindwa kuonyesha uwezo wa juu katika msimu uliomalizika hivi
karibuni chini ya Kocha Hans van Der Pluijm.
Minziro, kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga,
amesema endapo Yanga itawaondoa wachezaji hao,
anaamini watamsaidia katika harakati zake za kuhakikisha JKT Ruvu inakuwa
vizuri msimu ujao.
“Nimesikia kuwa Yanga wanataka kuwafungashia
virago wachezaji hao kwa madai kuwa wameshuka viwango, kama vipi wanipatie
mimi, siyo mmoja au wawili, nawataka wote,” alisema Minziro.
0 COMMENTS:
Post a Comment