Unamkumbuka
yuko kiungo mchezeshaji wa zamani wa Mtibwa Sugar na Yanga, Abdi Kassim ‘Babi’,
bado anaendelea kung’ara nchini Malaysia.
Wikiendi hii
ameingoza timu yake ya UiTM FC kuichapa Sabah FC kwamabao 3-1.
Babi akiwa
nahodha, El Hadji Diouf raia wa Senegal akiwa nahodha wa Sabah FC, bado hakuweza kuzuia makali
ya kikosi cha Mtanzania huyo.
Diouf ni mmoja wa wachezaji nyota barani Afrika na amewahi kung'ara akiwa na Liverpool na Bolton akikipiga nchini England.
Akizungumza
kutoka Al Shah Alam, Malaysia Babi amesema wamekuwa na mwendno mzuri ingawa si
sana.
“Ligi ni ngumu
na tunaendelea kupambana, baada ya ushindi huo dhidi ya kina Diouf tumesogea
hadi nafasi ya nane sasa,” alisema.
Tayari Babi
ameishatupia mabao nane nyavuni na ndiyo kiungo tegemeo wa UiTM FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment