Neymar ataikosa mechi ya Uefa Super Cup wakati
Barcelona itakapoivaa Sevilla, kesho.
Pamoja na mechi ya kesho, Neymar ataikosa pia mechi ya
Super Cup ya Hispania Barcelona itakapocheza dhidi ya Athletic de Bilbao.
Neymar analazimika kuzikosa mechi zote mbili kutokana
na kuwa majeruhi.
Kocha Luis Enrique ametangaza kumuengua Neymar ili
apate matibabu sahihi.
Lakini amesisitiza juhudi zinafanyika ili kuhakikisha
anarejea dimbani wakati wa mechi yao ya
ufunguzi wa La Liga wakatapotua uwanjani Jumapili Agosti 23 kuwavaa
Athletic Bilbao.
0 COMMENTS:
Post a Comment