Mtanzania Emily Mgeta
anayekipiga katika timu ya daraja la tano nchini Ujerumani sasa ameamua kujifua
zaidi kwa staili ya aina yake.
Mgeta aliyewahi kukipiga Simba ambaye ni beki
tegemeo wa Neckarsulmer, juzi alifanya mazoezi na timu ya Rugby katika eneo
analoishi.
“Kweli, niliamua kwenda
kwenye rugby kwa ajili ya kujiweka fiti. Siku hiyo hatukuwa na mazoezi, sasa
nikaona hakuna sababu ya kukaa tu.
“Nikaenda zangu pale na
kuomba nafasi ya mazoezi, kwa kweli nilijifua vizuri na kupambana na wale jamaa
unatakiwa kuwa imara kweli,” alisema Mgeta.
0 COMMENTS:
Post a Comment