Juhudi za
Kamati ya timu ya soka ya taifa, Taifa Stars bado zinaendelea kuhakikisha
inapatikana sehemu sahihi kwa ajili ya kambi kujiandaa kuing’oa Algeria kuwania
kucheza Kombe la Dunia.
Zimetajwa
kuwa ni Afrika Kusini na itakuwa katika mji tulivu wa Pretoria, Oman katika
jiji la Muscat au Dubai ndani ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Katibu na
msemaji wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda alisema bado mazungumzo na
vyama vya soka nchi hizo yanaendelea na mambo yakikaa sawa, watatangaza ni nchi
gani kikosi kitaenda kuweka kambi.
“Bado
mazungumzo na FA za nchi ambazo tumeaona ni pa zuri pa kuweka kambi
yanaendelea, hivyo mambo yakikaa sawa, muda wowote tutawatangazia ni wapi
kikosi chetu kitaweka kambi yake,” alisema Mapunda.
Kwa upande
mwingine, aliwaomba Watanzania kuisapoti kamati yao yenye jukumu la kuhakikisha
Algeria inachapwa pamoja na ukubwa wa jina lake kwenye soka barani Afrika,
ikiwa kileleni kwa ubora.
“Tunaomba
Watanzania kutupa mchango wa Sh 100 ambazo zinakwenda kufanya mambo mbalimbali
kama kuboresha kambi ya kikosi, motisha kwa wachezaji, chakula na mambo mengine
kama sehemu ya kuandaa mazingira mazuri ya timu,” aliongeza Teddy.
Kiasi hicho
kitumwe katika namba: 0654 888 868 au 0789 530 668.
Kamati hiyo
ipo bado inaendelea na mazungumzo kwa ajili ya kupata ndege ya kukodi kwa ajili
ya Watanzania watakaotaka kwenda kuisapoti Stars katika mchezo wa marudiano
huku Algeria. Nauli itatangazwa baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment