Kocha Abdallah Kibadeni ameanza kwa mkwara kazi
ya kuinoa JKT Ruvu kwa kufumua kikosi cha kwanza ambapo mabadiliko hayo
yaliiwezesha timu hiyo kutoka suluhu na Mtibwa Sugar juzi Alhamisi.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa
kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Kibadeni alikuwa anaiongoza timu
hiyo kwa mara ya kwanza huku akiwa amefanya mabadiliko kadhaa.
Kibadeni amemtumia Shaaban Dihile kwa mara ya
kwanza kikosini akichukua nafasi ya Hamis Seif, pia kiungo Issa Ngao naye
amejumuishwa kikosini kwa sasa.
Kocha huyo aliyewahi kucheza na kuifundisha
Simba, amesema huwa anawatumia wachezaji waliofanya vizuri mazoezini siku tatu
kabla ya mechi.
“Hiki kikosi unachokiona kilichocheza leo
(juzi) dhidi ya Mtibwa, karibu chote nimekifanyia mabadiliko, baadhi wanacheza
kwa mara ya kwanza na wengine nimewabadilisha nafasi ili tupate ushindi,”
alisema.
Licha ya matokeo hayo, bado JKT Ruvu ipo mkiani
mwa ligi kuu ikiwa na pointi mbili tu katika mechi saba ilizocheza hadi sasa.
Kibadeni amechukua nafasi ya Fred Minziro aliyejiuzulu kutokana na matokeo
mabovu ya timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment