HASSANOO AKIWA MAHAKAMANI KISUTU. HII ILIKUWA NI MIEZI KADHAA ILIYOPITA ALIPOKATALIWA DHAMANA. |
Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Hassan Othman 'Hasanoo' ameachiwa kwa
dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kukaa mahabusu kwa
muda wa miaka mitatu.
Hasanoo
aliwekwa ndani akikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo kosa la kuhujumu
uchumi na kusafirisha pembe za ndovu zenye thamani ya Sh bilioni 1.1
kwenda Hong Kong, China.
Mbali
na kesi hiyo pia anakabiliwa na kesi ya wizi wa tani 26.475 za madini ya Shaba
zenye thamani ya Sh 333, 467,848.13 kutoka Zambia kinyume na kifungu cha sheria
namba 258, 265 na 269 (C) vya kanuni ya adhabu mali ya Kampuni ya Liberty
Express Tanzania Ltd ambayo ilifunguliwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka
wa serikali DPP.
Mahakama
hiyo ilikubali kumuachia kwa dhamana baada wadhamini wa Hasanoo kukidhi vigezo
vya dhamana vilivyowekwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment