Premier League imezidi kushika umaarufu wa juu kutokana na kiwango kikubwa cha malipo ya haki za TV nje ya England.
Kwa sasa Premier League kupitia msimu wa 2016 hadi 19 itaweza kuingiza hadi paunik bilioni 3.2 wakati wakati inaanza kujulikana kwa jina hilo msimu wa 1992-93 ilikuwa inaingiza kitita cha pauni milioni 8 tu kwa haki za kuonyeshwa kwa dunia nzima.
Marekani ndiyo wanaonekana kulipa fedha nyingi zaidi kwani watatoa hadi pauni milioni 109.6 wakifuatiwa na nchi za Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwa ndani ambao wanamwaga pauni milioni 98.6.
Umaarufu wa ligi hiyo umekuwa ukizidi kupaa kwa kasi na kuchangia kuziongezea klabu hizo kiwango kikubwa cha faida kupitia haki hizo za uonyeshaji wa mechi za Ligi Kuu England.
0 COMMENTS:
Post a Comment