Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limezifungia klabu vigogo wa Real Madrid na Atletico Madrid kufanya usajili wowote hadi wakati wa majira ya koto yaani Julai 2017.
Madrid imefungiwa kusajili ikiwa ni siku moja tu baada ya kocha wake mpya, Zinedine Zidane kuweka wazi kwamba anataka kumsajili kiungo wa Juventus, Paul Pogba.
Hali hiyo imetokana na Madrid na Atletico kukiuka vipengele vya usajili kanuni ya shirikisho hilo.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji kadhaa ambao walitakiwa kuuzwa au kujiunga na Madrid na Atletico wataathirika na uamuzi huo wa Fifa.
Hata hivyo, Madrid imetoa uamuzi wa klabu kwamba utakata rufaa kuhusiana na uamuzi huo wa Fifa kuwafungia.
Watakaoathirika kutokana na kufungiwa huko kwa Real Madrid na Atletico Madrid ni hawa wafuatao.
Real Madrid:
Gareth Bale (Anahusishwa kwenda Man United)
Cristiano Ronaldo (Anahusishwa kwenda Man United na PSG)
David de Gea ( Real)
Eden Hazard (Kujiunga Real)
Paul Pogba (Kujiunga Real)
John Stones (Kujiunga Real)
Harry Kane (Kujiunga Real)
Robert Lewandowski (Kujiunga Real)
Atletico Madrid:
Antoine Griezmann (Anahusishwa kwenda Chelsea)
Saul Niguez (Anahusishwa kwenda Man United)
Jackson Martinez (Anahusishwa kwenda Chelsea)
Diego Costa (Kujiunga Atletico)
Odion Ighalo (Kujiunga Atletico)
0 COMMENTS:
Post a Comment