Na Saleh Ally
Kabla ya mechi ya watani, Yanga na Simba juzi Jumamosi, washambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib na Hamisi Kiiza ndiyo walioonekana kuwa hatari zaidi.
Ajib na Kiiza waliiongoza Simba kushinda mechi sita mfululizo za Ligi Kuu Bara, hivyo kuonekana kama washambuliaji tishio huku wenzao Donald Ngoma na Hamisi Tambwe wakionekana kusuasua kwa kuwa ndani ya mechi sita, Yanga ilipoteza moja na kuambulia sare moja.
Hata hivyo katika mechi hiyo, Kocha Jackson Mayanja wa Simba, alilazimika kuwatoa kipindi cha pili.
Wachezaji hao walishindwa kuonyesha cheche hata kidogo na kuingia katika kundi la wachezaji waliochemsha katika mechi hiyo.
Kiiza na Ajib, hata shuti moja la maana kwao kuonyesha kwamba walikuwa hatari hawakuweza kupiga.
Mashuti waliyoiga yalikuwa dhaifu na wenyewe wakaonekana laini na rahisi kwa ngome ya Yanga, tofauti na ilivyokuwa ikionekana awali.
Pamoja na kwamba beki Abdi Banda alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 25, bado wawili hao hawakuonekana kuwa msaada kwa Simba, hali ambayo si kawaida yao kabisa.
Huenda ingekuwa rahisi kwa mmoja kushindwa kutamba, lakini wote wawili, walikuwa “nyanya” hasa.
Mgema akisifiwa tembo hulitia maji!Mliwasifu sana kiasi cha kuanza kupandisha mabega wakati uwezo wao ni hafifu mno!
ReplyDelete