March 15, 2016


Msanii maarufu wa muziki kipya, Ambwene Yessayah ‘AY’ ambaye ni shabiki mkubwa wa Barcelona ya Hispania amewacharua mashabiki wa Arsenal kwa kutupia picha mtandaoni ikionyesha shabiki ambaye anajisomea.

Shabiki huyo wa Arsenal anajisomea namna ya kuikwepa Barcelona ambayo wanakutana nayo kesho katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

AY

Mechi hiyo itapigwa kwenye Dimba la Camp Nou jijini Barcelona huku tayari Barcelona ikiwa na faida baada ya kushinda mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 ugenini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV