March 19, 2016- Dakika za mwisho, wakati Coastal Union wanatafuta bao, lakini Simba wanagongeana 'kishkaj' kusubiri muda uishe ili waondoke na pointi zao tatu na kujichimbia zaidi kileleni

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA

SUB Dk 90, anatoka Kazimoto, nafasi yake inachukuliwa na Mussa Hassan Mgosi
 Dk 88, Coastal Union wanapata kona baada ya Agban kufanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 80 hadi 83, sasa Simba wanagongeana kwa 'shoo' huku Coastal Union wakiwa wanautafuta mpira
Dk 76 hadi 79 mpira unaendelea kuchezwa katikati zaidi, Simba wanaupoozeesha wakionekana kuvizia zaidi muda uende. Nje, anaonekana Paul Kiongera akipasha
SUB Dk 75 Anaingia Awadhi Juma kuchukua nafasi ya Ndemla

Dk 74, Ndemla anapoteza nafasi nzuri kabisa ya kufunga akiwa katika eneo la 18, ilikuwa ni baada ya Lyanga kutoa pasi nzuri kabisa kwake
Dk 66, Juma Mahadhi anapoteza nafasi nzuri kabisa kwa Coastal Union baada ya kipa Agbani kwenda kuokoa lakini yeye anashindwa kufunga

Dk 63, Kiiza anatoa pasi nzuri kabisa kwa Lyanga lakini Lyanga anakuwa na papara, anapiga shuti nyanya na kipa anadaka kwa ulaini
KADI Dk 58, Juuko alambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mahadhi
DK 53 HADI 56 Simba wanaonekana kuridhika na bao hizo mbili, sasa wanapiga pasi nyingi ambazo si kwa lengo ya kufanya mashambulizi tena, hili si jambo jema kwao

GOOOOOOOOOO Dk 52, Kiiza anaandika baso safi kabisa kwa kichwa. Ilikuwa ni baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Nimubona kutoka kulia. Ni bao la 16 kwake msimu huu

KADI Dk 47, Hamadi Juma analambwa kadi ya njano kwa kucheza kibabe, tena bila sababu
Dk 46, Lufunga analazimika kutoa mpira na kuwa kona baada ya kubanwa na Chiedebere aliyeingia katika kipindi cha pili
MAPUMZIKO
-Dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, Simba wanaonekana kuizidia zaidi Coastal ana kufanya mashambulizi mengi
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
DK 44, Tshabalala anapiga shuti kali kabisa, kipa anautema, mpira unawakuta Kiiza na Lyanga, wanaugombea na badala yake wanapoteza. Kama wangekuwa na mawasiliano, ingekuwa rahisi mmoja kumuachia mwingine na kuandika bao la pili kwa Simba
GOOOOOOOOOOO Dk 39, Lyanga anaifungia Simba bao safi kabisa baada ya kuunganisha krosi nzuri ya Tshabalala, naye anaruka juu na kuunganisha kwa kichwa na kuifunga timu yake ya zamani

Dk 38, Kazimoto anapata nafasi na kutoa pasi nzuri kabisa kwa Kiiza, lakini anapiga shuti nyanya linalodakwa kirahisi

Dk 33 hadi 37, hakuna timu iliyofanya shambulizi kali. Badala yake mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi kila timu ikipiga pasi nyingi hasa Simba
Dk 32, pasi nzuri kabisa ya Mwinyi Kazimoto, inakuta Lyanga, anaachia shuti kali linagonga mwamba na kurudi uwanjani
KADI 30 Dk Yossouf Sabo wa Coastal Union analambwa kadi ya njano kutokana na kumrukia Lyanga

Dk 26, Tshabalala anapiga tena krosi safi, Coastal wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa na Ndemla, mchezaji mmoja wa Coastal Union anaunawa hapa mwamuzi anasema twende
Dk 23, Mkude anapiga shuti kali kabisa lakini anashindwa kulenga lango, goal kick

Dk 23, krosi nzuri kabisa ya Tshabalala, Coastal Union wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa na Tshabalala tena lakini Coastal wanaokoa
Dk 19 sasa, bado inaonekana Simba hawajawa na mashambulizi makali, ingawa wao ndiyo wametawala zaidi katika sehemu ya kiungo. Coastal Union wanashambulia kwa kushitukiza zaidi

Dk 16, Ndemla anaingia vizuri katikati ya mabeki wa Coastal lakini anapiga shuti nyanya kabisa
Dk 15, Lyanga analambwa buti gotini mbele ya mwamuzi msaidizi lakini anaonekana kutojali. Sasa Lyanga anatolewa nje kutibiwa
Dk 11, Simba wanagongena vizuri tokea langoni mwao hadi lango la Coastal lakini wanaonekana kutokuwa makini na mipango ya mwisho
Dk 8, kipa Agban anafanyiwa madhambi kwa makudi na mshambuliaji Shiboli na mwamuzi anamuonya kwa maneno
Dk 5, Coastal wanafanya shambulizi zuri kabisa, lakini wanashindwa kufanya umaliziaji baada ya kipa Agbani kupangua na mpira kurudi uwanjani
Dk 2, Kazimoto alikuwa anachambua lakini anaangushwa na mwamuzi anasema mpira upigwe kwenda Coastal, hata hivyo hakuna shambulizi la maana

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV