May 28, 2016


Marcus Rashford ameweka rekodi ya kuwa mshambuliaji kijana zaidi wa England kufunga bao katika mechi yake ya kwanza ya timu hiyo.

Rashford ambaye ni mwanafunzi, amefunga bao lake la kwanza akiichezea England kwa mara ya kwanza jana wakati ilipoivaa Australia.

Pia anashikilia rekodi ya mchezaji kinda wa tatu kuwahi kufunga akiwa na England baada ya Wayne Rooney na Michael Owen.MAMA MZAZI WA RASHFORD AKISHANGILIA BAO LA MWANAYE AKIWA JUKWAANI.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV