May 19, 2016


Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, kinachuka dimbani leo mjini Goa kucheza mechi yake ya tatu ya michuano ya vijana ya AIFF.

Serengeti Boys wanashuka kucheza dhidi ya timu ngumu ya Korea Kusini ambayo imeonyesha makali katika mechi zake za mwanzo.

Kwa upande wa Boys, katika mechi zao mbili za mwanzo, walianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Marekani, mechi ya pili wakawatoa shoo wenyeji India kwa kuwachapa mabao 3-1.


Leo ni kazi dhidi ya Wakorea, moja ya timu inayopewa nafasi ya kubeba ubingwa wa michuano hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV