June 19, 2016


Unaweza kusema kweli damu ya soka imo kwenye familia ya Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Yeye ndiye shabiki mamba moja wa APR ya Rwanda, lakini ni shabiki namba moja wa timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama Amavubi, yaani manyigu.

Lakini kama hiyo haitoshi, mwanaye Ian Kagame ameonyesha uwezo hadi kuchaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chino ya miaka 20.


Ian unamuona akiwa katika kikosi hicho cha U20 cha Rwanda ambacho kilicheza dhidi ya Morocco kwenye Uwanja wa Amahoro mini Kigali, hive karibuni.

Pia usisahau, Kagame ni shabiki mkubwa wa kikosi cha Arsenal kutoka England na ana urafiki na Kocha Arsene Wenger.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV