August 22, 2016

Ikicheza dhidi ya Real Sociedad huku ikiwakosa washambuliaji wake, Cristiano Ronaldo na Karim Benzema, usiku wa kuamkia leo ilianza vizuri msimu mpya wa 2016/17 kwa kupata ushindi wa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

Staa wa mchezo huo alikuwa ni Gareth Bale ambaye alifunga mabao mawili na kuipa Madrid pointi tatu sawa na wapinzani wao wakubwa, Barcelona ambao nao walishinda katika mchezo wao wa kwanza juzi.

Bale alianza kufunga katika dakika ya pili wakati la pili aliliweka wavuni katika dakika ya 90, huku lile la pili likiwekwa wavuni katika dakika ya 40 kupitia kwa kiungo chipukizi Marco Asensio.


Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane iliingia katika mchezo huo kwenye Uwanja wa Anoeta ikiwakosa Ronaldo ambaye bado hayuko fiti kutokana na kuwa katika hatua za mwisho kupona jeraha la goti alilopata alipokuwa akiichezea Ureno kwenye fainali yaE uro 2016 wakati Benzema bado hajawa fiti kutokana na kujiunga na wenzake akiwa amechelewa kutoka kwenye mapumziko.







Ronaldo anatarajiwa kurejea uwanjani wiki ijayo katika mchezo dhidi ya Celta Vigo. Wengine waliokosekana kikosi ni Pepe, Luka Modric na James Rodriguez

Wababe wengine wa Jiji la Madrid, Atletico Madrid walipoteza pointi mbili baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Alaves.


Mchezo huo ulikuwa mgumu katika muda wote ambapo Atletico ilipata bao lake katika dakika ya 90 kupitia kwa Kevin Gameiro, lakini wakati wakijua mchezo utamalizika kwa bao hilo, wageni hao walisawazisha katika dakika za nyongeza na kufanya matokeo kuwa 1-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic