August 19, 2016STAA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, juzi aliamua kutumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha mashabiki wake jinsi alivyokuwa akiwasili mazoezini akiwa na gari lake aina ya Bugatti Veyron lenye thamani ya pauni milioni 1.7 (Sh bilioni 3).

Mara baada ya kuweka video hiyo fupi, Ronaldo aliandika maelezo "Ninarejea nyumbani." huku akionekana kuwa mwenye tabasamu pana ndani ya gari hilo lenye uwezo wa kukimbia kilometa 255 kwa saa moja. 

Inaelezwa kuwa Ronaldo ambaye amerejea mazoezini hivi karibuni baada ya kupewa muda wa ziada kutokana na ushiriki wake katika Euro 2016, anamiliki magari 19 ambayo yote yana thamani kubwa na yapo jijini Madrid.

Baadhi ya magari mengine ambayo nyota huyo ambaye inaelezwa kuwa analipwa pauni 300,000 (Sh milioni 840) kwa wiki ndani ya Real Madrid, anamiliki ni Rolls Royce lenye thamani ya pauni 305,000 (Sh milioni 851) na Lamborghini Aventador lenye thamani ya pauni 240,000 (Sh milioni 700).


Mataji ya Lionel Messi ngazi ya klabu: La Liga (8) Supercopa (7) Copa del Rey (4) Ligi ya Mabingwa Ulaya (4) UEFA Super Cup (3) Klabu Bingwa Dunia (3)

Waliofunga mabao mengi chini ya Luis Enrique ndani ya Barcelona: Lionel Messi (100) Luis Suarez (85) Neymar (70) 

Lionel Messi amefunga mabao 26 dhidi ya Sevilla, ni idadi kubwa kuliko wapinzani wote aliowafunga.

Tangu kuanza kwa mwaka 2016, Lionel Messi amehusika katika mabao 52 ya Barcelona, amefunga 35, asisti 17.

Juzi, Thomas Vermaelen alianza kuichezea Roma, juzi, mechi yake ya kwanza tu akapewa kadi nyekundu dakika ya 41.


A photo posted by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV