April 1, 2019


Wakati Ibrahim Ajibu akiwa amebakiza miezi michache Yanga tayari kumaliza mkataba wake, inaelezwa vigogo wa Simba wanaendelea kumalizana naye kimyakimya.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema wamejidhatiti kuhakikisha anarejea ndani ya uzi mwekundu na mweupe kuhakikisha anacheza msimu ujao akiwa na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Imeelezwa kuwa vigogo hao wako kwenye mipango ya kumrejesha Ajibu huku ikisemekana anaweza akapewa mkataba wa miaka miwili.

Kuna uwezekano mkubwa Ajibu akarudi Simba kutokana na hali ya mpito ambayo Yanga wanapitia hivi sasa.

Tayari Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa hana shida na mchezaji yoyote Yanga anayetaka kuondoka aondoke kwani msimu ujao wamejipanga kufanya usajili wa maana.


7 COMMENTS:

  1. Jee ndoto zako za kusajili nyota wa kitaifa na kutokana na hali tete ya tanga inaweza kutimizwa kutegemea hela ya bakuli na huku yakihitajika mabilioni ya shilingi kuendeshea timu pamoja na mastaa unaowaota kuwasajili. Hali ya kipatio cha yanga mwaka jana ni bora kuliko mwaka huu na mwaka huu ni bora kuliko mwakani na mambo yatapopinduka usiingie mitini ukaiwacha yanga kizani. Fikiri vizuri kabla ya kutamka na usitamke kuwa upo tayari kila atakayetaka kuondoka aondoke. Wa kale walitamka Samaki akioza usimtupe, umtafutie viungo umkaushe, au atakuja kumuokota mwenzio ulie uje ujute.

    ReplyDelete
    Replies
    1. utakuwa umesahau kuwa Yanga ipo kabla hujazaliwa, wamepita nyota wengi sana pia imeshawahi kutimua timu nzima mfano ilipozaliwa Pan African na hv karibuni walipoibuka akina anuar awadh, silvanus ibrahim na nk

      Delete
  2. We ulitaka abembeleze wachezaji.?hivyo ndio sahihi mchezaji kama unaona timu haikufai ondoka.abembelezwe ye nani

    ReplyDelete
  3. Kiukwel hal ya yanga ni mbaya hata wachezaj wamevumilia mno kwangu mm naona zahera anatakiwa kutumia lugha ya upole ili wachezaj awatie moyo maana kila mmoja yupo kimaslah asiseme anataka kuondoka aondoke ilhal upende wa pili wanakula vzr ko inawauma nan hapend raha?

    ReplyDelete
  4. Atakimbia uyo maana mwakan tutampga mkono

    ReplyDelete
  5. Hivi Ajibu kuondoka Yanga ndiyo ishu gani?Habari yenyewe hii ya kusemekana, kuotea tu wala haina uhakika..Wataumia sana wakimkosa Ajibu!wakati huo simba itakuwa inachekelea!

    ReplyDelete
  6. Jamani muwe mnasoma hizi stori za Redio mbao kwanza kabla ya kulipuka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic