April 21, 2019



MANCHESTER United leo kwa mara ya kwanza wameonja joto ya kichapo cha mabao 4-0 ugenini kwenye Ligi Kuu ya England wakiwa ugenini mbele ya Everton uwanja wa Goodison Park.


Hiki ni kichapo cha kwanza kwa Meneja mpya wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjær  baada ya kupewa mkataba mnono wa miaka mitatu huku akiwa haamini kile anachokiona baada ya mpira kumalizika.

Mabao ya Everton yalipachwikwa na Richarlison dakika ya 13 na Gylif Sigurosson dakika ya 28 na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili Everton waliwaongezea kasi Manchester United na wakaongeza mabao mengine mawili ambayo yalipachikwa kimiani na Luka Digne dakika ya 28 na Theo Walcot dakika ya 64.

Leo Manchester United walizidiwa kila idara kwani mpaka mpira unakwisha walikuwa wamepiga shuti moja lililolenga lango huku wapinzani wao Everton wakiwa wamepiga mashuti ya hatari nane yaliyolenga lango, kwa upande wa kona Manchester United wamepiga kona mbili huku Everton wakipiga kona 10. 

Everton pia walianza vizuri kwa kutawala mpira zaidi ya wapinzani wao Manchester United ambao walifli kwenye umiliki leo hasa eneo la ulinzi ambalo lilikuwa dhaifu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic